WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO YATOA TAARIFA KUHUSU SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE KITAIFA

Na.Issack Gerald
Mkoa wa Katavi umeendelea kutajwa kuwa kinara wa mimba za utotoni kwa asilimia 45.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi Magreth Mussai wakati akizungumza na waandishi wa habari  Mjini Dodoma,kuhusu Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani.
Bi Magreth Mussai ametaja mikoa mingine inayoongoza kuwa mimba za utotoni baada ya Mkoa wa Katavi kuwa ni Tabora (43%),Dodoma (39%),Mara (37%) na Shinyanga (34%).
Katika hatua nyingine taarifa ya utafiti ya hali ya ukatili dhidi ya watoto iliyotolewa  mwaka 2011,inaonyesha kwa  kila watoto wa kike 3 mtoto 1 sawa na asilimia 27.9 amefanyiwa vitendo vya ukatili huku takribani asilimia 6.9 wakilazimishwa kufanyiwa ukatili wa kingono.
Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika siku ya mtoto wa kike duniani ni pamoja na kutoa elimu ya kujitambua  na  afya ya uzazi ili watoto wa kike wajilinde na mimba za utotoni.
Kabla ya maadhimisho hayo,kutakuwepo Kongamano la Wazazi,walezi,viongozi wa dini na watu mashuhuri watakaojadili changamoto za malezi kwa mtoto.
Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2014 inaonyesha kuwa asilimia 11 ya wanawake waliojifungua walikuwa na umri kati ya miaka 15 -19 .
Wakati huo huo Utafiti wa Afya ya Uzazi na Utoto na Viashiria vya Malaria (TDHS) wa mwaka 2015 unaonyesha asilimia 27% ya watoto wa kike wanapata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 18.
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike  Serikali kwa kushirikiana na wadau imeanza kutekeleza  Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2018 -2021/2022). 
Mpango huu umelenga kupunguza ukatili dhidi ya watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22 na tunatarajia kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 5.
Maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa Mkoani mara Oktoba 11 mwaka huu,yatakuwa na kaulimbiyu isemayo‘’Tokomeza Mimba za Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda’’. 

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA