ASKARI WA WANYAMAPORI MKOANI KATAVI WATUHUMIWA KUUWA NA KUJERUHI

MTU mmoja amepoteza maisha kwa madai ya kupigwa risasi na askari wa maliasili  na wengine wanne kujeruhiwa katika kitongoji cha Mnyamasi wilayani Tanganyika mkoani Katavi,wakati wa oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyamasi Bw.Magosha Mtoveka amesema tukio hilo ambalo lilianza juzi na kuendelea mpaka jana pamoja na askari hao wa maliasili kupiga ovyo risasi za moto pia vyakula na mali nyingine inaelezwa zimechomewa ndani ya nyumba zao.
Awali imedaiwa askari walifika kijijini hapo na kuanza kuwafurusha wakazi wa eneo hilo kwa kutumia nguvu na silaha za moto kwa madai kuwa wamevamia hifadhi ya msitu wa Msaginya.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda Dokta Theopista Elisa amekiri kupokea majeruhi kadhaa hospitalini hapo japo hakutaka kuthibitisha kuwa majeruhi hao wametokana na oparesheni hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuwa na utulivu
Miezi ya hivi karibuni maeneo mbalimbali ya mkoa wa katavi yamekuwa yakikumbwa na aina kama hii ya matukio hali amabyo mamlaka za serikali zinadai zinatimiza majukumu yake.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA