WANANCHI MKOANI KATAVI WAASWA KUMUENZI NYERERE KWA KUDUMISHA AMANI

Ikiwa kesho ni kilele cha mbio za mwenye wa uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Hayati Julius Nyerere,wakazi Mkoani Katavi wamesema kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa  Mwl.Julius Kambarage Nyerere inafaa kutumika kuyaenzi kwa kudumisha amani na mshikamano .

Kwa nyakati tofauti wamesema uzalendo wa Baba wa Taifa umeliunganisha taifa na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa utambulisho wa Mtanzania.
Aidha wameongeza kusema kuwa viongozi wa sasa wanapaswa kueendelea kudumisha demokrasia ikiwemo kuheshimu katiba ili kuendeleza dhana ya utawala bora ambayo muasisi wake ni hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Zoezi la kuuzima mwenge wa Uhuru visiwani  Zanzibar  litafanyika kesho katika viwanja vya amani  huku likiwa sambamba na  kumuenzi baba wa Taifa Mwl.julius Kambarage Nyerere ambapo kumbu kumbu hiyo hufanyika kila ifikapo tarehe 14mwezi October.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA