SHEIKH PONDA AJISALIMISHA CENTRAL POLISI

Sheikh Issa Ponda
Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central.
Kiongozi huyo wa dini aliwasili leo katika kituo hicho cha polisi akiwa na wakili wake Abdallah Safari ambapo ni kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.
Kamanda Mambosasa siku ya jana alimwagiza Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyotoa.
Kwa mjibu wa kamanda huyo,Sheikh Ponda alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo atakamatwa.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA