KILELE WIKI YA VIJANA,VIJANA MKOANI KATAVI WASHAURIWA KUJIAJIRI

BAADHI ya vijana katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamewashauri vijana wenzao kufanya kazi kwa bidii kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana hapa nchini.

Vijana hao wakiwemo Goodluck Valanti na Ngosha Doni wamesema kuendelea kusubiri kuajiliwa hakutawasaidia kuondokana na umaskini na badala yake vijana wajitambue kwa kufanya kazi  kwa malengo.
Kilele cha wiki ya vijana hutoa nafasi kwa jamii na serikali kujadili masuala ya vijana ilikwemo masuala ya kiuchumi ambapo serikali imekuwa ikihamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili wawezeshwe kujikwamua kiuchumi.

Wiki ya vijana hapa nchini hadhimishwa sambamba na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru pamoja na kumbuku ya kifo cha Hayati Julius Nyerere kila ifikapo Oktoba 14 kila mwaka ambapo kaulimbiyu  mwaka huu inasema ‘’Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu’’. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA