TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KATAVI TANZANIA

Na.Issack Gerald-Katavi
WILAYA ya Mpanda Mkoani Katavi imekumbwa na tetemeko dogo la ardhi ambalo halijajulikana ukubwa wake.

Tetemeko hilo ambalo athari zake hazijajulikana limetokea leo saa 3:05 asubuhi na kuzua taharuki kwa wakazi wa wilaya ya Mpanda kutokana na mtikisiko wa nyumba zao ambapo baadhi ya wakazi wamesema walikuwa ndani.
Baadhi ya maeneo ambayo mpaka sasa yameripotiwa kuguswa na tetemeko hilo ni mpanda mjini na baadhi ya kata zilizopo vijijini kama Kakese,Katumba na Mwamkulu.
Mwezi Mei mwaka huu kulitokea matetemeko kadhaa ambapo kwa mjibu wa wataalamu wa jiolojia hapa nchiniwalisema ni kutokana na mikoa ya Rukwa,Kigoma na Katavi kupitiwa na bonde la ufa lililopo katika ziwa Tanganyika. 
Hata hivypo huenda maeneo mengi ya Mkoa wa Katavi yakawa yameguswa na tetemeko hilo ambapo mpaka sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA