RAIS MGABE AMETUMBULIWA

Rais Robert Mgabe
Shirika la afya duniani WHO limefuta uteuzi wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,kama balozi wa nia njema wa WHO.
Awali alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma Lakini wakosoaji walisema mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka nchini humo chi ya utawala wa Mugabe wa miaka 30.
Wafanyakazi mara nyingi hukosa kulipwa na madawa wakati mwingine hukosekana huku Mugabe mwenyewe mwenye umri miaka 93 akiwa anasafiri nje ya nchi kupata matibabu.
Bw.Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya WHO.
Alisema anasalia kujitolea kufanya kazi na nchi zote na viongozi wake kujenga huduma bora za afya.
Uteuzi wa Bw.Mugabe ulipatwa na shutuma kali kutoka nchi za Serikali ya Uingereza,waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kukosoa uteuzi huo.
Kufuatia kukosolewa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa mataifa mengi wanachama,WHO haikuwa na lingine ila kufuata mpango wake wa kumvua Robert Mugabe wadhifa wa balozi wa nia njema.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA