MKUU WA SHULE MKOANI RUKWA AMEJIUA KWA KUKATA KOROMEO LAKE

NKASI-RUKWA
MKUU wa shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichoma kisu kwenye koromeo kutokana na wivu wa kimapenzi. 

Akizungumzia tukio hilo mratibu wa elimu kata ya Mtenga Hebron Mwafungo alisema mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake majira ya saa 6 siku ya ijumaa.
Alisema mwalimu huyo jana alikwenda kazini kwake shule ya sekondari Mtenga na baada ya majira ya saa 5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe nyumbani  na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake
Aidha alisema mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake wakike nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake huyo  mbali na nyumbani kwake na baada ya kurudi aliona damu zimetapakaa sebuleni na baada ya kuchungulia chumbali alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja ndipo alipotoa taarifa uongozi wa kijiji hicho.
Alisema baada ya kumuhoji mdogo wa marehemu huyo alisema kuwa kaka yake  siku za nyuma alikua na mgogoro na mkewe akimtuhumu kuwa si muaminifu katika ndoa yao lakini walizungumza na kuumaliza mgogoro huo. 
Siku chache baadaye mke wa marehemu huyo aliondoka nyumbani na kwenda mjini Namanyere bila kumuaga mume wake huenda jambo hilo lilimkasilisha kaka yake na kufikia uamuzi wa kujichinja.
Diwani wa kata ya Mtenga Pankrasi Maliyatabu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa baada ya tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Nkasi.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa George Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nakuongeza kuwa bado uchunguzi wa polisi unafanyika kufuatia tukio hilo. 

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA