WAKUU WA MIKOA 10 AKIWEMO WA KATAVI WAAGIZWA KUSIMAMIA ZAO LA KILIMO-Septemba 10,2017

Majaliwa ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wakuu hao
wa mikoa,katika kikao alichokitiisha mjini Dodoma ili kujadili mbinu za kufufua
zao hilo.
Majaliwa amesema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba
kuanzia maandalizi ya shamba,kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa,kuvuna,kutafuta
masoko ambapo amewataka wasimamie katika maeneo yao ili kilimo cha zao hilo kibadilike.
Wakulima wa pamba wamekuwa wakilalamikia bei kubwa ya pembejeo
ambazo husambazwa na mawakala,huku wakipewa baada ya mavuno wakipewa bei ambayo
hailingani na gharama za uzalishaji.
Wakulima wamekuwa wakilalamikia kuuziwa mbegu ambazo hazioti na
hakuna fidia ambayo hulipwa.
Wakuu wa mikoa waliohudhuria kikao hicho ni kutoka
Shinyanga,Singida,Kagera,Tabora,Morogoro,Mara, Mwanza,Simiyu,Katavi na Geita.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments