RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA PAMBA KIWE KINAFANYA KAZI-Septemba 10,2017

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kuhakikisha wamekikarabati ili kiweze kuanza tena uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambuzi wa Pamba na kutengeneza ajira kwa vijana mkoani hapo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa maika zaidi ya 20 hakifanyi kazi.
Alisema kuwa baada mwezi mmoja huo kukamilika atafanya ziara Kiwandani hapo ili kuhakikisha kama ukarabati umeshakamilika na mitambo imeshaanza kufanya kazi na kinyume cha hapo atalazimika kumwandikia Waziri wenye dhamana na viwanda ili wamiliki wake wanyang’anye kwa ajili ya kumpa mwekezaji mwingine.
Mwanri aliwaagiza Wamiliki wa Kiwanda hicho ambao ni Rajani pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kupanga ratiba ya mpango kazi wa utekelezaji shughuli zitakazoonyesha mipango ya ufufuaji na muda wa ukamilishaji kwa ajili kufanikisha zoezi hilo ndani ya muda ulipangwa , vinginevyo watashindwa.
Mmoja wa Wabia katika Umikili wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga Urveshi Rajani alisema kuwa watahakikisha kuwa ndani ya mwezi mmoja Kiwanda hicho kinakuwa tayari kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambaji wa zao hilo.
Alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanahamasisha wakulima kulima pamba kwa wingi ili Kiwanda cha kiwe na malighafi za kosha kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta na uchambuzi wa zao hilo.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Jospeh Mihangwa alisema kuwa mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Mananga ni mizuri na inasaidia kuchamba pamba bila kukatakata na hivyo kuwa na soko kubwa duniani.
Alisema kuwa kwa sababu ya ubora wa kiwanda hicho wao kama majirani na Mkoa wa Tabora wako tayari kushirikiana na wamiliki wake kama watahitaji msaada wa mafundi wa kusaidia kukarabati mitambo ili kianze tena uzalishaji kwa sababu kiwanda hicho ni muhimu sana katika uchambuzi wa pamba.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Revocatus Kuuli aliwahakikishia Wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manongo wasiwe na wasiwasi kuhusu upatikanaji malighafi ya kutosha kwa ajili ya kiwanda hicho,kwani uongozi umeshajipanga kuhakikisha msimu ujao wananchi walima Pamba kwa wingi na wanavuna pamba nyingi kuliko ya msimu uliopita.
Alisema pamoja na jitihada kuwa za muda mfupi msimu uliopita Wakulima katika Wilaya ya Igunga walifanikiwa kuzalisha kilo 10, 700,000 ,msimu ujao wanatarajia mavuno kuwa mara mbili ya kilo hizo na hivyo kuwa malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda..
Kiwanda hicho kinamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kwa asilimia 20 na M/S Rajani Metals and Machinery Ltd mwenyewe anamikili asilimia 80.
Kiwanda cha Manonga ambacho kilijengwa mwaka 1958 na Kampuni ya wafanyabiashara binafsi na mnamo mwaka 1962 Serikali ilikitaifisha na kuipatia Kampuni ya Wakulima wa Kahama na Nzega (KANZECO) kina miaka zaidi ya ishirini bila kufanya kazi.

 Habari zaini ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA