WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI YAANZA,WAZAZI KATAVI WAASWA KUNYONYESHA KWA MUDA WA KUTOSHA KWA AJILI YA AFYA ZA WATOTO-Agosti 2,2017

Ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi wa nane,wazazi  mkoani Katavi  wametakiwa kuwanyonyesha watoto mpaka wafikiapo umri wa miaka miwili ili kulinda afya zao. 

Muuguzi wa kituo cha afya cha Town Clinic katika halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi Lugalata Elias amesema  ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji maziwa,  wazazi wanatakiwa kufuata ushauri wanaopewa na watoa  huduma ili kuepuka kudhoofika kwa afya ya mtoto.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na kutofata  ushauri wanaopewa na watoa huduma hupelekea madhara kwa mtoto ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupungua kilo pamoja na kupata ugonjwa wa kilibatumbo.

Kwa upande wa wazazi wameeleza kuwa kutowanyonyesha watoto kwa wakati au kuwaachisha mapema,  ni kutokana na  mazingira magumu wanayopitia katika kipindi cha unyonyeshaji.  


Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA