WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WAUNGA MKONO DAWA ZA CHANJO KWA WATOTO ZICHUNGUZWE KUTOKANA NA WATOTO KULEWA,KUANGUKA NA KUZIMIA WANAPOTUMIA DAWA HIZO-Agosti 2,2017

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameunga mkono hoja ya baadhi ya madiwani waliotaka ziangaliwe upya dawa za chanjo zinazosababisha wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kuzimia baada ya kunywa dawa hizo.

Wakazi hao wakiwemo,John Pasua, Bi.Matengenezo Rafiki wa Elia na mama Mariam,wamethibitisha kwa nyakati tofauti kushuhudia na kusikia wanafunzi wakipatwa na tatizo la kuanguka mara baada ya matumizi ya dawa hizo.

Hatua ya kutaka dawa ziangaliwe upya iliibuka jana kupitia mkutano wa baraza la madiwani wa kufunga mwaka 2016 wa bajeti ambapo imeonekana kuwa takribani wanafunzi 16 wameanguka na kuzimia baada ya kutumia dawa hizo na hatimaye kufikishwa vituo vya huduma za afya.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kupitia mkutano huo amesema kuanguka kwa wanafunzi ni matokeo ya maudhi madogomadogo yanayotokana na dawa hizo ambazo kimsingi hazina madhara.


Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA