OFISI ZA WANASHERIA AKIWEMO MTOTO WA RAIS FATUMA KARUME NA LAURENCE MASHA ZATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO-Agosti 26,2017

Sehenu ya majengo ya Ofisi
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo.

Mkondya amesema Jeshi la polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko ambapo amesema hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA,Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani  ya ofisi hizo zilizopo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.
Aidha Fatma Karume ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar,Amani Abeid Karume ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo.
Wakaazi wa eneo hilo katikati mwa mji wa Dar es Salaam wamesema walisikia misururu ya milipuko mikubwa muda wa saa nane usiku na muda mchache baadaye jumba hilo likajaa moshi na vifusi.
Kampuni hiyo inaorodhesha kampuni za mawasiliano, kawi,benki pamoja na serikali kama mojawapo ya wateja wake.
Kufuatia tukio hilo,Rais wa chama cha mawakili wa Tanganyika Tundu Lissu ameshutumu shambulio hilo kama shambulio dhidi ya uhuru wa mawakili Lakini maafisa wa polisi wamesema kuwa ni mapema mno kusema kuwa lilikuwa shambulio la bomu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA