MANISPAA YA MPANDA YAPATA HATI SAFI UDHIBITI HESABU ZA SERIKALI,RC APONGEZA-Agosti 26,2017

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Msaafu Raphael Mugoya Muhuga

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga  ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Mpanda kwa kupata hati nzuri  ya udhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka 2016.

Muhuga ametoa pongezi hizo wakati wa  kikao maalumu cha baraza la Madiwani la Manispaa ya Mpanda kilicholenga kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Aidha amewaomba waendeleze juhudi za kuhakikisha wanapata hati zinazoridhisha ili kusudi Mkoa upige hatu katika masuala ya Maendeleo kwani hati ni kipimo na  kigezo cha kuonesha halimashauri inafanyaje.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda katibu tawala wa wilaya hiyo Bw. Sostenes Mayoka licha ya kuipongeza manispaa amesema katika kupata hati safi kitengo cha ukaguzi wa ndani ni Muhimu hivyo ameshangazwa na taarifa inayoonesha kitengo cha Ndani Ni Dhaifu. 
Hata hivyo pamoja na kwamba Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda imepata hati safi ya udhibiti wa hesabu za serikali ,katika ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka 2015/2016 iliyosomwa na Christopher Sinkamba kwa niaba ya mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu Mkoani Katavi Bw.Gerald Machumu,inaonesha Manispaa imeshindwa kutekeleza masuala mbalimbali ikiwemo kuchangia Shilingi Milioni 159,723,059.30 kama asilimia 10 katika mfuko wa wanawake na vijana,kutochangia asilimia 40 sawa na shilingi milioni 480,519,976.60 kwa ajili ya maendeleo ya vijijini.
Mapungufu mengine yanalenga katika matumizi ya fedha bila kupita katika idara husika,utata katika kukabidhi wa gari la kuzoa taka kwa Halmshauri ya Manispaa lenye thamani ya Shilingi Milioni 92,760,000 kwa zaidi ya miezi 29 gari ambalo lilinunuliwa mwaka 2016 pamoja na ukusanyaji dhaifu wa fedha kutoka baadhi ya vyanzo vya mapato.
Kwa mjibu wa mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za serikali Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kwa mwaka 2013/2014 ilipata hati safi,2014/2015 hati isiyoridhisha na 2015/2016 imepata hati inayoridhisha.
Hatua ya kuwasilishwa na kujadiliwa ripoti mbalimbali za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali ni utekelezwaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alilolitoa Aprili 22 mwaka huu akiwaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha hoja zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG zikiwemo hoja za miaka ya nyuma pamoja na maagizo ya Kamati ya bunge ya kudumu ya serikali za mitaa (LAAC) zinapatiwa majibu na kufutwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA