RTO KATAVI:WAMILIKI IMARISHENI MAGARI YENU KABLA YA SAFARI-Agosti 9,2017

Wamiliki wa magari katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani katavi wametakiwa kuhakikisha magari yao yanakuwa imara kabla ya kuyaigiza barabarani.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa usalama barabarani mkoani Katavi John Mfinanga wakati akizungumza kuhusu operesheni ya ukaguzi wa magari ilianza kwa lengo la kuhakikisha magari yanakuwa imara na salama kabla ya kuanza safari ili kuzuia ajali za barabarani.
Mfinanga amebainisha kuwa operesheni hii ni endelevu na endapo watakamata magari mabovu hayataruhusiwa kusafirisha abiria kwenda eneo lolote mpaka wamiliki wataka po yatengeneza .

Operesheni hii ni ya nchi nzima na kwa mkoa wa dar salaam inajulika kwa jina la nati kwa nati wakati mkoa wa katavi ikijulikana kwa jina la nati kwa boliti.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA