OPARESHENI BOMOABOMOA YAENDELEA KULIZAWAKAZI MKOANI KATAVI-Agosti 9,2017

WAKAZI wa kitongoji cha Mgolokani Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kurejeshewa ardhi yao au kuwatafutia maeneo ya kuweka familia zao kufuatia kufukuzwa na nyumba zao kubomolewa ambapo serikali imedai kuwa wakazi hao wanaishi ndani ya misitu ya hifadhi.

Wakazi hao wakiwemo Bi.Grace Aloyce na Leonard Maembe,wakizungumza na Mpanda Radio,wamesema mpaka sasa wanalala nje huku baadhi ya mali na vyakula vya familia vikiwa vimepotea wakati wa oparesheni ya kubomoa makazi yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Mkogokani Bw.Divason Kisulo,amesema wamekuwa wakiishi katika eneo hilo tangu mwaka 1974 ambapo amesema zaidi ya kaya 200 zimebomolewa makazi yao na kusababisha zaidi ya watu 1, 075 kuathirika kwa kukosa mahali pa kuweka familia zao pamoja na upotevu wa mali.
Hata hivyo kutokana na kutompata mkuu wa Wilaya ya Mpanda ili kuzungumzia mgogoro huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kusema hawezi kulizungumzia suala hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga akiwa safarini,ameiambia Mpanda Radio kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Mpanda atafuatilia uhalali wa eneo hilo.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA