WATANZANIA 96 WAFADHILIWA KIMASOMO NA NCHI YA UHOLANZI-Julai 28,2017



Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi inchini humo.

Ufadhili huo wa Watanzania 96 ni kutoka Serikalini, sekta binafsi na asasi za kiraia,wamenufaika kimasomo kutoka seriklai ya Uholanzi ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali hiyo kuchangia maendeleo nchini.

Akiongea katika ghafla fupi ya kuwaaga Watanzania hao, iliyofanyika  katika ukumbi wa Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam, Balonzi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe.  Jaap Frederiks alisema kwamba Serikali ya Uholanzi kwa muda mrefu imekuwa ikichangia miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Balozi Jaap alieleza kuwa Watanzania waliofaidika na mpango huo unaojulikana kama Netherlands Fellowship Programme – NFP, ni waajiriwa kutoka Serikalini, sekta binafsi, wafanyabiashara wadogo pamoja na waajiriwa kutoka Asasi za kirai.

“Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa moja kati ya wafaidika wakubwa wa ufadhili wa Masomo Nchini Uholanzi program inayojulikana kama “Netherlands Fellowship Programme – NFP” ambapo zaidi ya Watanzania 5000 wamefaidika na ufadhili huo katika kozi mbalimbali”. alisema Mhe. Balozi Jaap.

Serikali ya Uholanzi imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo baadhi ya Watanzania pamoja na kuboresha Sekta ya rasilimali watu, tukiamini kwamba kupitia watu hao tunachangia katika maendeleo ya Taifa.

Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi nchini humo


Habari zaidi P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA