WA CCM AMBWAGA WA CHADEMA UCHAGUZI NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA,KAMATI ZA KUDUMU NAZO ZAPATA WENYEVITI WAKE-Julai 27,2017



HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoa Katavi,imemchagua Mh.Theodola Romwad Kisesa wa chama cha Mapinduzi CCM kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya kuchaguliwa kwa kura 17 dhidi ya kura 4 za Mh.Issack Lusambo wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Akitangaza Matokeo hayo katika Mkutano mkuu wa mwaka wa fedha 2016/2017,mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mjibu wa sheria.
Kwa upande wao baadhi ya wenyeviti wa kamati ambao wamechaguliwa wakiwemo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi,uchumi na mazingiraTeddy Petro Nyambo ambaye ni diwani viti maalumu tarafa ya Karema na mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji Mh.Frank Lugasi ambaye ni diwani wa kata ya Tongwe wamesema wamejipanga kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ili kushughulikia matatizo ya wananchi.
Wakati huo huo Juma Kassim amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya madiwani.
Hata hivyo kwa mjibu wa sheria na kanuni za uatawala hapa nchini,viongozi wa kamati ya Ardhi na kamati ya bodi ya Ajira hudumu katika uongozi kwa miaka mitano tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA