WAKAZI WA INYONGA WILAYANI MLELE WAENDELEA KULIA NA TATIZO LA UKOSEFU WA UMEME-Julai 11,2017

WAKAZI wa Kata ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwapelekea umeme wa uhakika ili kuchochea maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.

Wakazi hao wakiwemo Zachari Efraim na Living James,wametoa ombi hilo leo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme na kupelekea shughuli za uzalishaji mali zinazotegemea umeme kukwama kwa mwaka sasa.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Inyonga Mh.Masoud Mbogo,amesema tatizo hilo amekwishalifikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Rafael Muhuga ambapo mkuu wa Mkoa aliahidi kulifanyia kazi kwa wakati.

Wakazi wa Inyonga hawana umeme tangu mwezi Julai mwaka jana,baada ya wafanyabiashara binafsi waliokuwa wakifua umeme kusitisha kwa madai kuwa wanaendesha mradi kwa hasara.

Hata hivyo mkakati wa mradi wa umeme wa REA unaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha wakazi wa kata ya Inyonga ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Mlele wapate nishati ya umeme.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA