MTOTO MCHANGA AOKOTWA SHAMBA LA MIGOMBA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA- Julai 11-2017.


Rangi ya kijivu ndipo Wilaya ya Kasulu inapopatikana Mkoani Kigoma

MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya wiki tatu na Mwezi mmoja wilayani Kasulu mkoani Kigoma ameokotwa katika  migomba  alipotelekezwa na mwanamke asiyejulikana na kutokomea kusiko julikana.

Mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Nyakitonto wilayani humo Bw Julius Baligela amesema  mtoto huyo wa njisi ya kike ameokotwa kwenye migomba jirani na mahame ya mtu mmoja akiwa amefungwa kanga.

Bw Baligela ameeleza kuwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi wasamalia wema walitoa taarifa wa uongozi na kisha kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya taratibu za kipolisi kukamilika na halamshauri imetoa gari kusafirisha mtoto kuyo kituo cha kulelea watoto Matyazo Kigoma.

Aidha Kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji  cha Nyakitonto kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kufanya uchunguzi  kumbaini mwanamke aliyehusika na kitendo hicho.


Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA