PIKIPIKI YAGONGA GARI MKOANI KATAVI,WATU 2 AKIWEMO DEREVA NA ABIRIA WAKE WANUSURIKA KIFO-Julai 27,2017



WATU wawili akiwemo dereva wa piki piki maarufu kama boda boda akiwa abiria wake,wamenusurika kifo baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kugonga gari.

Tukio hilo limetokea jana maeneo ya Mpanda Hotel barabara ya Kigoma baada ya dereva wa pikipiki hiyo ambaye alitoroka baada ya ajali hiyo kujaribu kulipita gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 334 AHD lililokuwa likisafirisha mazao kuelekea katika maghala ya kuhifadhia nafaka.
Wakizungumza katika eneo  la tukio,baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo halisi cha tukio hilo ni uzembe uliofanywa na dereva wa gari hilo kutokuwasha Taa za zinazoonesha upande anakokatisha.
Mmoja kati ya majeruhi waajali hiyo ambaye amejeruhiwa kichwan,mguuni,na mikononi aliyejitambalisha kwa jina la Ngosha,ameelezea tukio hilo ambapo amesema amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kwa upande wa Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani PC John Shindika akizungumzia tukio hilo,amesema ametoa wito kwa madereva wote wakiwa barabarani kuzingatia sheria kuepuka ajali.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA