MANISPAA YA MPANDA YATOA MAJIBU KUHUSU WAKAZI WA MSASANI WATAKAOBOMOLEWA MAKAZI YAO : WASIO NA UWEZO WATAPEWA VIWANJA MTAA WA KAMPUNI,WENYE UWEZO KIASI WATALIPA KIDOGOKIDOO VIWANJA VILIVYOPIMWA-Julai 27,2017



HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imetenga viwanja vilivyopo katika mtaa wa Kampuni Kata ya Misunkumilo kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msasani watakaobomolewa makazi yao ambapo pia imesema watakaohitaji kupata viwanja vilivyopimwa ndani ya Manispaa watalazimika kulipa nusu ya gharama na kiasi kingine kulipwa baadaye.

Hatua hiyo imethibitishwa na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo kupitia kikao cha baraza la madiwani wakati akijibu hoja za madiwani akiwemo diwani wa kata ya Mpanda Hotel Mh.Willium Liwali waliotaka kufahamu hatua iliyokwishafikiwa na Halmshauri katika kuwasaidia wahanga wa bomoabomoa.
Hatua ya kupata maeneo ya kuwapeleka wakazi wa mtaa wa Msasani watakaobomolewa nyumba zao ni utekelezwaji wa agizo la mkuu wa Wilaya ya Mpanda alilolitoa Wiki iliyopita akimwagiza mkurugenzi Manispaa ya Mpanda kutafuta viwanja kabla ya miezi sita kuisha.
Zaidi ya nyumba 200 za wakazi wa mtaa wa msasani zinazodaiwa kuwa ndani ya mipaka ya hifadhi ya reli zinatarajiwa kubomolewa ifikapo mwenzi Januari mwakani.
Habari zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA