WANNE MBARONI KWA UUZAJI WA GONGO NA BANGI KATAVI



WATU wanne mkoani Katavi wamekamatwa kwa makosa tofauti likiwemo la uuzaji wa Gongo  na debe moja la Bangi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda wakati akizungumza na Mpanda radio juu ya matukio yaliyotokea mkoani hapa hivi karibuni.
Aidha Nyanda amewataka wananchi kuacha kujihusisha na biashara haramu kama njia ya kujipatia kipato badala yake wajishughurishe na biashara halali katika kujipatia kipato.
Sanjari na hayo amsisitiza kuwa watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili hatua zichukuliwe dhidi yao na iwe fundisho kwa wengine.
Matukio ya uuzwaji wa madawa ya kulevya na vitu visivyo halali kisheria vimekuwa vikiuzwa Mkoani Katavi.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA