HALMSHAURI ZA WILAYA YA MPANDA NA TANGANYIKA ZATAKIWA KUTENGA 5% YA MAPATO KWA AJILI YA WAJASILIMALI VIJANA




Na.Richard Mbeho-Mpanda
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda na Tanganyika zimetakiwa  kutenga asilimia 5 za mapato ya ndani kwa ajili ya kuwasaidia vijana kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya vijana Wilaya za Tanganyika na Mpanda wakiwa kati mikutano ya hadhara(PICHA NA.Issack Gerald)
                                                        

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wabaraza la Umoja wa Vijana  wa CCM Bw. Stephano Mwakabafu  ambae   pia ni diwani wa kata ya uwanja Ndege katika kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zinazowakbili vijana wa mkoa Katavi.
Aidha Bw. Mwakabafu amewataka pia vijana hao kuunda vikundi ili kuweza kupatiwa mikopo itakayowasaidia kuongeza kipato  na  kuondokana na umaskini.
Kwa upande wa baadhi ya vijana walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa viongozi wamekuwa wakiahidi kuwasaidi fedha lakini hawaoni utekelezaji wake.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA