WAJASILIMALI KATAVI WATAKIWA KUTUMIA ELIMU YA UJASILIMALI WANAYOPATA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO KUJIKWAMUA KIMAISHA



Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WAJASILIAMALI wametakiwa kutumia elimu ya ujasiliamali wanayopewa katika mafunzo ili kujikwamua kimaisha.
Wajasilimali wanawake baada ya somo la mafunzo ya ujasiliamali(PICH ANA.Issack Gerald)
                                              

Rai hiyo imetolewa na  Afisa maendeleo ya jamii wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Marietha Mlozi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda wakati  akifungua semina ya siku tatu ya ujasilimali ambayo inafanyika Mpanda Mjini.
Aidha amewasisitiza kuendelea kuunda vikundi ili kukidhi vigezo vya kukopesheka katika bajeti ya Halmashauri na fursa nyingine za mikopo zinapopatikana.
Nao baadhi ya wajasiliali ambao wameshiriki katika semina hiyo wamesema watatumia elimu ya ujasilimali wanayopewa ili kufanya shghuli zenye tija.
Semina hiyo ya siku tatu ambayo imeanza leo inatarajia kumalizika Jumatano ya wiki hii ambapo miongoni mwa wawezeshaji wa semina hiyo ni Shirika la ANAMED ambao ni muunganiko wa dini mbalibali hapa nchini.
Hata hivyo changamoto ambayo bado inawakabili wajasiliamali baada ya mafunzo ni ukosefu wa mitaji,teknolojia ya kisasa katika ufungashaji wa bidhaa na masoko.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA