WALIOANZISHA MAKAZI KIHOLELA KATIKA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI KUONDOLEWA KWA NGUVU,WAKUU WA WILAYA WAPEWA RUNGU NA MKUU WA MKOA


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Mugoya Muhuga akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake(Hawapo pichani)(PICHA NA.Issack Gerald) Agosti 3,2016

Waandishi wa habari Mkoani Katavi wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 3,2016
                            
Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda.Safu yote ya chini ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi wake ambapo Safu ya Juu ni Ofisi za Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda na watumishi wake(PCHA NA.Issack Gerald) Agosti 3,2016
                                                       
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga ametoa agizo wa wakazi Mkoani Katavi wanaoishi katika hifadhi za wanyama,misitu ya hifadhi na maeneo yasiyo rasmi kuondoka wenyewe kwa hiari kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema ametoa agizo hilo ili kunusuru misitu inayoendelea kuteketea kutokana na uanzishwaji wa makazi mapya na ufyekaji miti ovyo.
Aidha Jenerali Muhuga kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari,amefanya kikao na wakuu wa Wilaya zote tatu za Mkoa wa Katavi na kuwaagiza kusimamia zoezi la kuwaondo wavamizi wa misitu na kuharibu Mazingira.
Hata hivyo amesema wakala wa kuhifadhi misitu Mkoani Katavi wana changamoto ya uhaba wa watumishi ambapo mpaka sasa kuna watumishi 21 kati ya 250 wanaohitajika na hivyo zoezi la kupambana na waharibifu wa mazingira na misitu kuwa migumu kwa kuwa hata vyombo vya usafiri hawana.
Wakati huo huo amesema mpaka sasa kuna kesi mbili zinazohusishwa na uharibifu ambapo katoi ya hizo kesi moja ni ya Afisa mtendaji wa katika serikali za mitaa aliyeruhusu watu kufyeka miti na kuanzisha makazi holela na kupelekea uharibifu wa mazingira.
Katika hatua nyingine,Mkuu wa Mkoa amekitangaza Kijiji cha Majalila kilichopo kata  ya Tongwe kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA