WAKUU WA IDARA ZA ARDHI MKOANI MWANZA OFISINI HAPAKALIKI,JINO KWA JINO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI


Na.Albert Kavano-Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongera Leo amezindua  program ya kushughulikia Migogoro ya ardhi mkoani humo na kuagiza  wakuu wa idara ya ardhi kutotoka nje ya wilaya wala kuingia ofisini siku ya jumanne badala yake wakae na kutatua migogoro hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw.John Mongera
                

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mkoa huo kuwa na migogoro ya ardhi isiyo malizika kutokana na utata wa umiliki wa ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza hali inayo sababaisha wengi kuzungukia ofisi za mkuu wa mkoa  na wakuu wa wilaya kwa matatizo ya ardhi.
Katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya hamashauri ya jiji Bw Mongera amesema kuwa katika malalamiko kumi sita ni ya ardhi, hivyo wakuu wa idara watatakiwa kufunga ofisi na kutafuta eneo ili kuwasikiliza na kushughulikia migogoro hiyo kabla ya kuwajibishwa wenyewe.
Aidha amewataka wananchi kuepuka tabia za utapeli wa kugushi nyaraka za umiliki wa ardhi na atakaye kuwa na nyaraka  bandia atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA