WAKAZI KIJIJI CHA ITENKA KUANZA UJENZI KITUO CHA POLISI



Na.Issack Gerald Bathromeo
Wakazi wa Kijiji cha Itenka kilichopo Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wametangaza kuanza ujenzi wa kituo cha Polisi katika kijiji hicho.
Baadhi ya akina mama katika mkutano wa kijiji(PICHA NA.Issack Gerald)

Taarifa ya mchakato wa ujenzi wa kituo cha polisi kijijini hapo,imetolewa na mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Marco Katambi wakati wa mahojiano na waandishi wa habari katika makao makuu ya kijiji hicho yaliyopo hapo Itenka.
Aidha Bw.Kitambi amesema,kwa muda Mrefu,kijiji cha Itenka hakina ulinzi imara ambapo askari huonekana tu siku ya mnada kuimarisha usalama katika mnada uliopo katika kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kongeza nguvu zaidi katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa wao wapo tayari kuchangia asilimia 20 wanazotakiwa kuchangia katika ujenzi wa maendeleo.
Mbali na kijiji hicho kutokuwa na kituo cha Polisi,wananchi pia wanasema wanakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa maji safi na salama,huduma za afya,shule,miundombinu ya barabara na ukosefu wa stendi kwa ajili ya maegesho ya magaari na pikipiki.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA