WAKAZI KIJIJI CHA KAKESE MANISPAA YA MPANDA WAELMISHWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

WAKAZI wa kijiji cha Mbugani kata ya Kakese Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameaswa kutunza vyanzo vya maji vilivyopo bonde la Mto Mpanda.
Picha na p5 tanzania
                                                   
Picha na P5 tanzania
                                                   

Rai hiyo imetolewa leo na  Afisa Maendeleo ya Jamii Tadeus Ndeseiyo wa idara ya maji na umwagiliaji  bonde la ziwa Rukwa       alipokuwa akitoa elimu katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika kijijini hapo.
Ndeseiyo amezitaja changamoto zinazohatarisha mto Mpanda  kuwa ni shughuli za kilimo na umwagiliaji pamoja na uchungaji mifugo unaoendelea pembezoni mwa mto huo.
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji wameeleza kutofahamu sheria ya kulima  mita sitini kutoka mtoni ili kulinda vyanzo vya maji hali ambayo elimu isipotolewa haraka kwa wananchi hawa huenda mto katika miaka mitano ukawa umetoweka.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo inakabiliwa na uharibifu wa mazingira hususani vyanzo vya maji.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA