MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA MBIYO ZAKE WILAYANI MLELE WAZINDUA MIRADI,WAPOKELEWA MANISPAA YA MPANDA


WAKAZI wa tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wametakiwa kutoziharibu barabara za mitaani katika tarafa hiyo zilizotengenezwa kwa kiwango cha lami.
                             

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa George Jackson Mbigima wakati wa Uzinduzi wa barabara zenye urefu wa KM 2 sanjali na  Miradi mbalimbali  katika Mbio za mwenge wilayani Mlele.
Ujenzi wa barabara hizo umetekelezwa na kutumia bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 ambapo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 710 ambazo zilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmshauri ya Wilaya ya Mlele.
Aidha Mbigima ameiomba Halmashauri ya Mlele kuwawezesha vijana kukidhi vigezo vya kukopesheka katika benki mbalimbali ili kuondokana na wimbi la kukaa vijiweni pasipo kufanya kazi na kupelekea kufanya uharifu.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Mlele Bw.Simioni Lwitiko Kasumo amesema Ujenzi wa Mradi huo  Umetekelezwa chini ya Mfuko wa Barabara wa Halmashauri pamoja na nguvu ya wananchi.
Mwenge wa uhuru Umepokelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi ukitokea katika Halmashauri Mpya ya Mpimbwe baada ya kupokelewa kutoka Mkoani Rukwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe Umezindua Miradi Mbalimbali ndani ya wilaya ikiwemo Mradi wa Maji Utakaowezesha kupunguza kero ya Maji kwa wakazi wa tarafa ya Inyonga.
Mwenge wa uhuru umewasili leo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda kuendelea na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo miradi ya maji,ujenzi wa barabara na vikundi vya kupambana na kuzuia Rushwa.
Mwenge wa uhuru ukiwa Mkoani Katavi unatembelea Jumla ya Halmashauri 5 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,Mlele,Mpimbwe,Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Tanganyika.
Mbiyo za mwenge wa uhuru mkoani Katavi zitahitimishwa Julai 14,2016 na kukabidhiwa Mkoani Kigoma kupitia wilaya ya Uvinza.
Kauli mbiyu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ‘’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,washirikishwe na kuwezeshwa’’
Mwandishi:Ester Lameck
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA