MIL.52 KUTUMIKA KUJENGA VYUMBA VYA SHULE YA MSINGI KASEKESE



SHULE ya msingi kasekese iliyopo kata ya kasekese wilaya mpya ya Tanganyika mkoani katavi wametengewa fedha kiasi cha shillingi milion 52 kwa ajili ya kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa mpanda  vijijini Mh.Suleman Kakoso baada ya kutembelea   kijijini hapo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kasekese kata ya Kasekese(PICHA NA Issack Gerald)
                                                         

Aidha Kakoso amewashukuru wananchi hao kwa kujitolea kujenga baadhi ya vyumba vya madarasa bila kuwepo kwa nguvu ya serikali ambapo amewaasa kutokata tamaa katika kuboresha miondombinu ya elimu kwa ujumla.
Shule nyingi zilizopo vijijini zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa vinavyoendana na idadi ya wanafunzi pia upungufu nyumba za walimu.
Mwa ndishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA