CHANGAMOTO LUKUKI ZAENDELEA KUKWAMISHA MAENDELEO YA WANANCHI KATA YA ITENKA.



Wakazi wa kata ya Itenka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoani Katavi,wameiomba Serikali ya halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo kutatua changamoto za miundombinu ya barabara kuanzia Mpanda Mjini hadi Itenka.

Kwa muda mrefu wakazi wa kijiji na kata ya Itenka eneo lililo kitovu cha uchumi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo wamekuwa wakisumbuliwa na changamoto lukuki zikiwemo za kutokuwepo kwa maji safi na salama ambapo katika huduma ya wanalazimika kunywa maji ambayo yanakanyagwa na watu wanapokuwa wanagombania maji hayo huku wanyama kama mbwa nao wakinywa maji katika visima hivyo vifupi ambavyo vimechimbwa na wananchi hao katika kuonesha jitihada za kutatua ukosefu wa maji.
Wakizungumza na Mpanda Radio kijijini Itenka kwa hisia kali za maumivu ambayo yamesnbabishwa matatizo waliyonayo kutokanana na kukosa huduma za jamii,wamesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Wilaya ya Mlele na mkoa wa Katavi wamekuwa kama wameisahau kata ya Itenka huku wananchi hao wakisisitiza kuwa kwa nafasi zao wako tayari kuchangia kwa asilimia 20 wanazotakiwa kuchangia isipokuwa wamekwamishwa na mipango ya serikali.
Changamoto nyingine ambazo zimetajwa na wananchi hao kukosekana kwa kituo cha afya na ukosefu wa stendi ya Magari ambapo mara kwa mara watu hunusurika kugongwa na magari hao sambamaba na pikipiki kutokana na kutokuwa na sehemu maalumu ya kupaki vyombo hivyo vya usafiri.
Wakitolea ufafanuzi kuhusu barabara inayoanzia Mpanda Mjini hadi Itenka,wakazi hao wamesema kuwa barabara imekuwa ikikwanguliwa na kuwekwa chanagalawe na changalawe kumomonyoka na kusambaa kutokana na kuonekana kujengwa chini ya kiwango na kuwa shida wakati wa masika ambapo mapaka sasa barabara yote imejaa mchanga hali inayopelekea magari na pikipiki kushindwa kupita hususani barabara kutoka Itenka kuelekea vijiji vya vya Imilamate na Mwamkalu.
Katika hatua nyingine wakazi wa Itenka,wameiomba serikali kuondoa mageti mengi yaliyowekwa barabarani karibu na mashamba yao ili kuwatoza ushuru kinyume na alivyoagiza Rais John Magufuli huku wakitaka kutofautishwa kati ya mkulima anayetoa mazao shambani na mfanyabiashara anayesafirisha mazao kwa ajili ya biashara.
Wamesema serikali inatakiwa kusimamia agizo la Mkuu wa Nchi Rais Dkt.John Pombea Magufuli aliyeagiza kuondolewa mageti yasiyo ya lazima barabarani yanayomnyonya mkulima na mfanyabiasahara ambapo Rais magufuli aliagiza kuondolewa kwa vizuizi barabarabani ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Bw.Joseph Raulence Mpemba amekiri kuwepo kwa changamoto hizo lukuki katika kata ya Itenka ambapo amesema kuwa katika sekta ya afya zimetengwa Shilingi milioni 70 kujenga kituo cha Afya kijijini Itenka kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Bw.Mpemba akizungumzia kuhusu kuwepo kwa mageti mengi amesema kuwa geti linalotakiwa kuwepo ni moja tu na siyo zaidi ya matano yaliyopo kwa sasa hali inayoleta utata kwa wakulima na wafanyabiashara ambapo kwa sasa wanalazimika kuchangia zaidi ya mara moja upande wa Nsimbo na Mpanda na kuendelea kujikita katika dimbwi la umaskini.
Aidha Bw.Mpemba amesema suala la maji ni tatizo kubwa na amethibitisha ukubwa wa tatizo ambapo huenda muda wowote magonjwa ya tumbo yakawakumba wakazi wa itenka kutokana na hali ya huduma ya maji ilivyo kwa sasa ikiwa serikali haitaweka mkono wako na kutupia macho yake kata hiyo.
Kata ya Itenka inasifika kwa shughuli za kilimo huku zao kubwa linalozaliwa zaidi na kukuza uchumi wa Halmashauri na Mkoa likiwa Mpunga ambapo changamoto hizo chanagamoto zinazowakabili wakazi wa itenka zinatakiwa kutatuliwa haraka ili kuongeza kasi ya maendeleo ya wananchi.
Katika hali halisi ya kauli mbiyu ya hapa kazi tu ikisimamiwa ipasavyo na Halmshauri,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkoa kama serikali ya awamu ya tano inavyoagiza ni wazi kuwa wakazi wa Itenka wataondokana na matatizo waliyonayo mara kilio cha wananchi kinaposikika.
Mwa ndishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA