LEO WAZIRI MKUU PINDA MGENI RASMI TUZO ZA WALIMU KATAVI



Na.Issack Gerald Bathromeo      
Leo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kutoa tuzo za kuwapongeza walimu wa shule za msingi zilizopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya kufaulisha Wanafunzi kwa ufaulu wa asilimia 90 hadi 97 kwa mwaka 2014 na 2015 na kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka miwili mfululizo kwa kufaulisha wanafunzi.
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda(PICHA NA.Issack Gerald
   

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Fransis Nzyungu amsema kuwa mgeni rasmi katika hafla hii anatarajia kuwa Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga amesema kuwa walimu hao wanatakiwa kupatiwa pongezi kwa kuwa wameleta heshima kubwa katika taifa hili la Tanzania kuanzia mwaka 2013 tangu ulipoanzishwa mpango wa Matokeo Makubwa sasa.
Mwanzoni mwa wiki hii,Mkuu wa idara ya elimu shule za msingi(Afisa elimu) Bw.Visent Kayombo alisema kuwa ufaulu kwa mwaka 2013 ulikuwa asilimia zaidi ya 62,2014 asilimia 90 na 2015 asilimia 97 ambapo hata hivyo akasema kuwa kulingana na mikakati iliyopo kwa sasa wanatarajia kufaulisha kwa asilimia 98 katika mitihani itakayofanyika 2016.
Wakati huo katika ngazi ya Mkoa,mkoa wa Katavi katika matokeo ya mtihani kwa mwaka 2014 ulishika nafasi ya tatu na 2015 kushika nafasi ya kwanza kwa kufaulisha wanafunzi wa shule za msingi kwa kiwango cha juu.
Hata hivyo manispaa ya Mpanda imekuwa ikifanya vizuri pia katika sekta nyingine ambapo kwa miaka ya hivi karibuni Manispaa ya Mpanda(Wakati huo hadhi ya mji) ilipata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kwa hapa nchini kwa kuwa mji msafi kuliko miji yote hapa nchini.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA