YALIYOMKUTA ALIYEKAMATWA NA JINO MOJA LA TEMBO MKOANI KATAVI LENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.1 HAYA HAPA



MTU mmoja mkazi wa Mgorokani Matandarani wilaya ya  Mlele mkoni Katavi amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda  kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kukutwa na jino 1 la tembo lenye thamani ya shilingi milioni thelasini.

Akisoma shtaka hilo mwanasheria wa serikali Bi.Jamira Mzilai  mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mh.Chigangwa Tengwa amemtaja mshtakiwa kuwa ni Stiven Ndangula (59).
Ameongeza kuwa mnamo  mei 5 mwaka huu katika eneo la mgorokani  wilaya ya mlele mshtakiwa alikutwa na makosa hayo ambayo ni jino la tembo pamoja na kukutwa na nyara za serikali bila kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.
Hata hivyo  mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa  mahabusu  kwa kukosa kukidhi  vigezo vya dhamana ambapo mahakama imeahirisha shtaka hilo  hadi litakapotajwa tena juni 23 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Vitendo vya watu kukamatwa na nyara za serikali Mkoani Katavi vimekuwa vikitokea mara kwa mara amabapo hata hivyo kwa kiasi kikubwa wahusika wamekuwa wakikamatwa.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA