WATANZANIA WAPYA KATUMBA WATAKIWA KUTOKARIBISHA WAGENI KINYUME CHA SHERIA



WATANZANIA waliopewa Uraia katika Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele, Mkoani Katavi, wametakiwa kuacha kuwakaribisha watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa katavi meja jeneral Mstaafu Raphael Muhuga wakati akiongea na Watanzania hao wapya Hivi karibuni waishio maeneo ya makazi ya wakimbizi ya katumba ambapo wametakiwa kuishi kwa Upendo na kuzingatia Sheria za nchi.
Meja Mhuga amebainisha kuwa Kumekuwepo na matukio ya Ujambazi hivi karibuni ambapo mtu mmoja anaedhaniwa kuwa jambazi ameuwawa na wengine wawili kushikiliwa na jeshi la polisi ambapo mmoja amekimbia na  kutokomea pasipojulikana.
Aidha mkuu wa mkoa  amekemea vitendo vya watanzania Hao wapya kufanya mazoezi ya kijeshi katika mapori yanayozunguka makazi hayo kwani kufanya ivyo ni kukiuka taratibu za nchi.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA