WIKI HII MAMA WA WATU JERA MIEZI SITA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA GONGO



Mahakama ya wilaya mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miezi sita jera au kulipa faini kiasi cha shilingi laki moja  kwa kosa la kukutwa na pombe haramu.

Akisoma hukumu hakimu  mfawidhi wa mahakama hiyo mh, Chiganga Tengwa  amemtaja mshitakiwa kuwa ni Mariam Mwanang’ombe (48) mkazi wa Tambukaleli kuwa alitenda kosa hilo mei 31 mwaka huu  asubuhi  Nyumbani kwake akiwa na lita 20 za pombe haramu  ya kinyeji aina ya gongo.
Kwa upande wake mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea amaiomba mahakama impunguzie adhabu kwani anaugonjwa wa kuanguka,ni mjane na anafamilia inayomtegemea.
Hivyo pombe hiyo imeharibiwa na mahakama imemhukumu ili  iwe fundisho kwa watumiaji na watengenezaji wa pombe haramu.
 Mwandishi :Vumilia Abel
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA