HUYU NAYE WIKI HII KADAKWA NA MENO MAWILI YA TEMBO WILAYANI MLELE,MWINGINE NAYE AIBA MPUNGA SHAMBANI AKAMATWA NA WANANCHI ACHOMWA MOTO HADI KIFO.



JUNI 14 mwaka huu,Jeshi la Polisi lilimkamata Oscar Pius Mizengo(30) mkazi wa Kitongoji cha Inyagala - Ikuba Kijiji cha Nyakasi kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi akiwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32 moja likiwa na urefu wa sentimita 150 na lingine 148 cm ambayo thamani yake ni Tsh 30,000,000/= milioni thelasini sawa na tembo mmoja aliyeuwawa.

Akithibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ambaye pia ni mratibu na mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoani SSP Focus Malengo alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Juni 10 mwaka huu katika Kitongoji cha Inyagala - Ikuba Kijiji cha Nyakasi kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
SSP Malengo alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa mtuhumiwa Oscar Pius anamiliki meno ya tembo na ndipo ufuatiliaji ulipoanza kwa kufanya upekuzi katika makazi yake na kufanikiwa kumkamata akiwa na meno hayo huku akiwa ameyahifadhi shambani kwake kwa kuyafukia chini.
Hata hivyo mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Katika hatua nyingine mwanaume aliyefahamika kwa majina ya Nhuli Nduta anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 53 hadi 40 aliuwawa na kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi wa mpunga ambao haujavunwa shambani.
Aidha, katika tukio hili Kamanda Malengo alisema hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusika na mauaji hayo ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Mnyagala linaendelea na misako mikali kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi alitoa wito kwa wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile uharibifu wa rasilimali za Taifa mfano vitendo vya ujangili uwindaji haramu kuacha mara moja na badala yake wajikite kufanya shughuli halali katika kujipatia kipato.
Mwandishi :Vumilia Abel
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA