KUHUSU UCHANGIAJI DAMU SALAMA WIKI HII MKOANI KATAVI,SERIKALI YA MKOA YATUPIWA LAWAMA KUTOUNGA MKOANO ZOEZI HILO



Juni 14 wiki hii ilikuwa ni kilele cha Siku ya uchangiaji damu salama kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu.
Miongoni mwa wahitaji wakubwa wa damu ni pamoja na mama wajawazito ,watoto wenye umri chini ya miaka   5 pamoja na wagonjwa mbali mbali wenye uhitaji wa huduma hiyo.

Kupitia kampeni hiyo ambayo ilianza Juni 1-14,2016,wananchi mkoani Katavi wemetakiwa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Hadija Juma Mtalaamu msaidizi wa wa damu salama Mkoani Katavi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mwitikio wa watu ulikuwa mdogo ambapo hakuna kiongozi yeyote ambaye alijitokeza kuunga mkono juhudi za uchangiaji damu salama.
Hata hivyo licha ya kuwa kulikuwa na mwitikio mdogo katika kilelele cha siku ya uchangiaji damu salama katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili,Hadija alisema kuwa katika maeneo mengine waliko fika mwitikio wa watu ulikuwa mzuri  ukilinganisha huku chanzo cha mwitikio mdogo ni uhamasishaji hafifu.
Kitaifa kilele cha maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama kilifanyika mkoani  Dodoma.
Serikali ilikuwa imeweka kiwango cha chupa zaidi ya 100 kukusanywa kutoka kila mkoa ili kupata damu ya kutosha kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA