WAKAZI KATA YA KAZIMA WALALAMIKIA MANISPAA YA MPANDA KUTOPIMIWA VIWANJA VYAO KWA MIAKA 9 SASA



Wakazi wa kata ya kazima manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa  halimashauri hiyo kushindwa kuwapimia viwanja takriban miaka tisa, hali iliyowalazimu baadhi yao kuanza ujenzi wa maeneo hayo bila kupimwa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika makao makuu ya kata hiyo wamedai kuwa baadhi ya wananchi walijitolea eneo la ekari 63 kwa ajili ya kupimiwa viwanja ambapo kaya 215 zilichangia kiasi cha shilingi 28,000.
Akijibu malalamiko hayo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya mpanda Bw. lauter kanoni amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano na kuahidi kushughulikia suala la upimaji wa eneo hilo lenye mgogoro wa muda mrefu.
Aidha afisa mtendaji wa Kata ya kazima Bi. Digna Nkana amekiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa muda mrefu na kuongeza kuwa suala hilo limechangia kuzorotesha maendeleo ya kata hiyo.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA