LATCU KATAVI WASHAURIWA KUWEKEZA UJENZI WA MAJENGO KUJIIMARISHA KIUCHUMI



MKUU wa mkoa wa Katavi meja generali mstaafu  Raphaeli Muhuga amesema chama kikuu cha ushirika cha  wakulima wa tumbaku LATCU  kinaweza kupata ufanisi zaidi kama kitaendeleza jitihada zake za kuwekeza katika ujenzi wa majengo kama vitega uchumi.

Meja generali mstaafu Muhuga amezungumza hayo katika kijiji cha Igagala wilaya ya Mpanda mara baada ya uzinduzi wa soko la Tumbaku uliojumuisha wakulima kutoka vyama mbalimbali vya ushirika.
Amesema kuwa ubunifu wa kuwekeza katika majengo ni mfano wakuigwa na mashirika  mengine ili kuwaletea tija wakulima.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha ushirika mkoani Katavi Bw Modestus Yamlinga amesema kuwa jumla ya kilo zaidi ya milioni 9 za Tumbaku zimevunwa katika msimu wa mwaka 2015/16 kwa mkoa mzima.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA