RIPOTI KAMILI YA TAKUKURU MKOANI KATAVI KUWABULUZA MAHAKAMANI WATU WATATU KATI YA WATANO HII HAPA


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Katavi TAKUKURU imewafikisha watu watatu katika mahakama ya wilaya ya  Mpanda kwa kosa la uhujumu uchumi.

Watu hao walifikishwa mahakamani kwa kukabiliwa na mashitaka matatu ambayo ni  ya kutumia nyaraka  na kumdanganya mwajiri,kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikari hasara ya zaidi ya shilingi milioni 61,159.40.
Mawakili na wanasheria wa Takukuru Mkoani Katavi Bw.Bahati Stafu Haule na Simon Buchwa waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Naomi Ndelelio Nnko Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia aliwahi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,Godfrey Athanase Majuto ambaye ni Mhandisi Mjenzi Halmshauri ya Manispaa ya Songea ambapo pia katika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda alikuwa ni Mhandisi Mkuu kitengo cha ujenzi.
Watuhumiwa wengine ni  Beatus Joseph Bisesa Mhandisi Ujenzi ya Ukandarasi ya Matoke Constraction Caompany na Mmiliki wa Kampuni hiyo ya Ukandarasi Mhandisi Chiyando Muyenjwa Matoke ambaye kwa sasa ni Mhandisi ujenzi Halmshauri ya Wilaya ya Kishapu pamoja na Petro Jurgen Mwanoni aliyekuwa Mhandisi Mchundo wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wakisomewa shitaka hilo na mawakilii pamoja na wanasheria wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Katavi mbele ya hakimu  mkazi mfawidhi Chiganga Tengwa,washitakiwa hao walikana kosa.
Mawakili na wanasheria hao waliiambia mahakama kuwa mnamo Tarehe 15/11/2012,Ofisi ya TAKUKURU mkoani Katavi ilifanya ilipokea taarifa iliyotuhumu kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa wa taratibu katika kutekeleza mradi wa barabara ya Kasokola-Mtapenda-Nsemulwa yenye urefu wa KM 22 wakituhmu kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda imezembea kusimamia mradi huo kwani Kampuni au mkandarasi ameshindwa kufanya kazi hiyo na badala yake kufanywa na kampuni au mkandarasi mwingine tofautikinyume na mkataba ambapo hata hivyo matengenezo ya barabara hiyo haikukidhi kiwango kutokana na fedha iliyokuwa imekwishakulipwa.
Aidha TAKUKURU mkoa wa katavi  imetoa wito kwa wanachi wote Mkoani Katavi kujiepusha na vitendo vya rushwa katika sekta za umma na za watu binafsi.
Washtakiwa watatu waliokuwepo mahakamani,wawili kati yao walikidhi vigezo vya masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ambao ni Naomi Ndelelio Nnko na Godfrey Athanase Majuto huku Chiyando Muyenjwa Matoke akiwekwa mahabusu hadi atakapotekeleza masharti ya dhamana hiyo.
Hata hivyo Watuhumiwa wote walikana mashtaka dhidi yao.
Mwandishi : Issack Gerald
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na  P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA