HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA YAZINDUA MNADA MPYA WA BULAMATA,ULINZI KUIMARISHWA SIKU ZA MNADA


HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda  Mkoani Katavi imezindua Mnada mpya wa mifugo wa Bulamata uliopo kata ya Bulamata ambapo pia bidhaa tofauti na mifugo zinatarajiwa kuuzwa katika mnada huo.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)
                           
Afisa Mifugo Halmshjauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Bulamata  na maeneo jirani wakati wa uzinduzi wa Mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Ng'ombe wakiwa mnadani siku ya uzinduzi wa a wa BulamataMnad(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Mmoja wa wapishi katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Mama akitengeneza kitoweo cha wateja  katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Baadhi ya wafanyabiasahara wadogo katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Afisa Mifugo Halmshjauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo akitoa taarifa ya Mnada wa Bulamata wakati wa uzinduzi wa Mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Mh.Augustino Sadick Mathew diwani wa kata ya Ilangu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Mh.Sikudhani Kolongo diwani viti maalumu diwani kata ya Mishamo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo akihutubia wakazi wa kijiji cha Bulamata wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Viongozi na wanakijiji cha Bulamata wakati wa uzinduzi mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)
Mbuzi akiwa katika mnada wa Bulamata aliyeletwa kuuzwa (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)
                                                      
Afisa mtendaji kijiji cha Bulamata Bw.Joseph Lusambo akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mh.Hamad Mapengo wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016)

Akizindua mnada huo,mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo,amewataka wafanyabiashara watakoatumia mnada huo kuutumia vizuri kwa ajili ya maendeleo.
Kwa upande wake Afisa mifugo Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo ametoa wito kwa wafanyabiasahara hasa wa mifugo kuzingatia kibali cha kuuza mifugo kutoka mamlaka husika ili kuthibitisha uhalali wa mifugo wanayotaka kuuza.
Wakati huo huo wakizungumza kuhusu usalama mnadani hapo,afisa mifugo Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda  Mh.Hamad Mapengo wametoa wito kwa vyombo vya usalama hususani kata za Bulamata na Mishamo kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo ili kuzuia wizi wa mali na fedha za wafanyabiashara.
Awali akisoma taarifa ya mnada huo,Afisa mtendaji kwa kijiji cha Bulamata Bw.Joseph Lusambo,amesema kuwa asilimia 85 ya wakazi wa kata ya Mishamo iliyogawanyika na kupata kijiji na kata ya Bulamata,wanajihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji ambapo pia amesema,kwa mjibu wa sensa ya wanayama iliyofanywa  na chama cha wafugaji kijijini hapo kwa mwaka 2012,ni pamoja na ng’ombe 19630,mbuzi 12,912, kondoo 273,ngururuwe 264,kuku 27491,bata 2126,mbwa 612,punda 61 na paka 465.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo msaidizi wa polisi kituo cha Mishamo,Afande Julius Chemka amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo siku za mnada.
Mmoja wa wananchi walikuwepo katika uzinduzi wa mnada wa Bulamata Bw.Wambura Ernest amesema anatarajia kuuza biashara yake kwa mafanikio kutokana na watu wengi kufika katika mnada huo kununua bidhaa mbalimbali.
Mnada huo wenye ukubwa wa ekari 100 unatarajia kuwanufaisha watu wapatao 6000 wanaozunguka eneo la mnada suala ambalo limepongezwa na wakazi wa kijiji cha Bulamata pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Mh.Frenk Kibigas diwani kata ya Tongwe,Mh.Augustino Sadick Mathew diwani kata ya Ilangu,Mh.Rehani Simba diwani wa Kata ya Ipwaga ,Mh.Sikudhani Kolongo diwani viti maalumu kata ya mishamo na diwani wa kata ya Bulamata.
Afisa Mifugo wa Halmshauri ya Wilay aya Mpanda Bw.Elikana Magambo amesema,kuzinduliwa kwa mnada wa Bulamata,kunakamilisha jumla ya minada 5 inayoiingizia kipato Hamshauri ya Wilaya ya Mpanda ambapo minada hiyo ni Sibwesa,Kapanga,Kapalamsenga,Mnyagala na Bulamata ambapo.
 Halikadhalika magulio matatu ya Mwese,Vikonge na Ilebula yametajwa kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya mapato vya Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mnada huo utakuwa unafanya kazi tarehe 10,11 na 28 ya kila mwezi.
Mwandishi : Issack Gerald
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na  P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA