WANANCHI WILAYANI MLELE WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA CHF


WANANCHI katika kata ya Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani katavi wametakiwa kuwa mabalozi katika maeneo mbalimbali katika uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya CHF.
                                                     

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mlele Godwini Beene wakati wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya CHF yaliyofanyika katika ofisi za kata ya ilunde wilayani humo.
Kwa upande wake meneja wa mfuko huo katika mkoa wa katavi Dk. Clement Massanja  lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kusaidia kaya kupata huduma bila malipo kwa kuchangia kiasi cha shilingi elf 10 kwa mwaka na kuwataka wananchi kuuamini mfuko huo kwani ndiyo mkombozi wao.
Katika zoezi hilo zaidi ya kaya 40 zimejiunga na mfuko huo hali ambayo inazidi kuiweka kata hiyo katika nafasi nzuri ya wananchi kujiunga na mfuko huo katika halmashauri  hiyo.
Mwandishi : Judica Schone
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na  P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA