WALIMU WAGOMA KUFUNDISHA WAKIPINGA MWALIMU MWENZAO KUPIGWA NA AFISA ELIMU,CWT KUTOA TAMKO LEO


WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.

Makamu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Kipesha alisema wameitisha mgomo huo wa siku mbili kupinga kitendo cha Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao Jacob Msengezi (25) ambaye anafundisha somo la Hisabati Darasa la Saba shuleni hapo.
Akifafanua,alisema walimu hawataingia kufundisha kwa siku hizo mbili na watakuwa ofisini wakiandaa mitihani huku wanafunzi wakiendelea kuhudhuria shuleni hapo kama kawaida.
Naye Mwalimu Msengezi aliliambia gazeti la Habari leo kwa akiwa shuleni Kianda kuwa juzi Jumatano Ofisa Elimu, Fusi alitembelea shuleni hapo saa tatu asubuhi akikagua mazingira ya shule na hatimaye kufanya kitendo hicho.
Katibu wa CWT Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Vicent Ndewele amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kuwa chama hicho kitatoa msimamo wake leo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA