SHILINGI MIL.1 YA MKOPO YATOLEWA NA MBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI KWA VIKUNDI 4 VYA WAJASILIAMALI KATA YA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA


Vikundi 4 kati ya 28 vya wajasiliamali vilivyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo vimekabidhiwa mkopo kwa Shilingi milioni Moja kwa ajili kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Mgeni rasmi katika makabidhiano ambaye ni Diwani wa kata hiyo Mh.Bakari Kapona ,akikabidhi hundi ya fedha hiyo kwa wajasiliamali hao kutoka mfuko wa Kata hiyo ambao umeanzishwa na Mbunge wa Mpanda Mjini Mh.Sebastian Kapufi,amevitaka vikundi hivyo kutumia fedha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa Katavi hiyo Bw.Jumbe Museluka amesema kuwa kila kikundi kimepata Shilingi laki mbili na nusu ambapo amewataka kuzirejesha fedha hizo kwa wakati ili vikundi vingine vipatiwe mkopo huo kila baada ya miezi mitatu.
Wakizungumza kwa niaba ya wanachama wenzao,viongozi wa vikundi hivyo pamoja na mambo mengine,wametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mh.Sebastian Kapufi kwa kuendelea kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi kwa mwaka 2015.
Makabidhiano hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi za Kata ya Nsemulwa zimehudhuriwa na Adam Masigati Mwenyekiti wa mtaa wa Nsemulwa,Emmanuel Luhamba mwenyekiti wa mtaa Kilimahewa Nsemulwa,Revocatus Pekewe wa mtaa wa Kichangani,Ahamad Kahena Makokolo sanjari na viongozi wa chama cha Mapinduzi ambapo  Kwa upande wake Christopher Simon Watujabo ambaye ni msemaji wa chama cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Nsemulwa akisema kuwa hueo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi inayofanywa na Mbunge Mh.Sebastian Kapufi pamoja na kuupongeza uongozi wa kata ya Nsemulwa kwa kuviandaa vikundi.
Shughuli mbalimbali ambazo zimeelezwa kufanywa na vikundi mbalimbali vya wajasiliamali katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na ufugaji wa kuku,biashara ndogondogo,kilimo ambapo wajasiliamali wa kata ya Nsemulwa walio wengi wameelezea kuhakikisha wanaondokana na ukali wa maisha kwa kutumia pesa kwa malengo yaliyokusudiwa huku wakisisitiza kuwa makini na baba wa familia kuzitumia fedha hizo kwa ajili ya ulevi.
Vikundi hivyo ni San Vela Group cha Kilimahewa,Smathday cha Nsemulwa,Iyombabuzoba cha Migazini na Ilakoze Group cha Mtaa wa Nsemulwa.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA