KIKOSI CHA JADI KIJIJI CHA KAWANZIGE MPANDA CHAAPISHWA KUAPMABANA NA UHARIFU



KIKOSI cha ulinzi wa jeshi la jadi maalufu kama sungusungu katika kijiji cha Kawanzige kata ya Kakese manispaa ya Mpanda kimeapa kuendelea na mapambano dhidi ya uhalifu katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa jana katika hafla ya kutathimini uwajibikaji wa makamanda wakati wa utekelezaji wa majukumu ya ulinzi na usalama katika kijiji hicho.
Katika risala iliyoandaliwa kwa mgeni rasmi jeshi hilo limeonekana kupata mafanikio makubwa katika dhana ya ulinzi pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Kwa upande wa jeshi la polisi ambao umewakilishwa na Zabron Ibeganisa kamanda wa polisi jamii mkoa wa Katavi  kwa niaba ya OCD amesema jeshi la polisi linatambua na kuthamini mchango mkubwa wa uimalishaji wa ulinzi shirikishi kwa kutumia jeshi la sungu sungu.
Kumekuwa kukijitokeza uharifu mwingi ikiwemo wizi wa mali za raia ikiwemo mifugo
Mwandishi:Alinanuswe Edward
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM pekee

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA