BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA USIKU WA KUAMKIA LEO MEI 21,LAPITISHA WATUMISHI 13 KATI YA 16 WALIOKUWA WAMESIMAMISHWA KAZI KUKATWA MISHAHARA KUFIDIA HASARA ILIYOTOKANA NA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MIRADI ZA MANISPAA,MMOJA AFUKUZWA KAZI,WENGINE WATUPIWA TAMISEMI IWAPANGIE INAKOTAKA MBALI NA MANISPAA


Baraza la madiwani katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,limepitisha maamuzi  ya kukata mshahara wa watumishi 13 kati ya 16,waliokuwa wamesimamishwa kazi na baraza hiloFebruari 26 mwaka huu,kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwemo utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa taka pamoja na ubadhilifu wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese ambapo pia watumishi watatu wameshushwa vyeo.

Uamuzi wa baraza hilo umetolewa usiku wa kuamkia leo Mei 21,2016 katika kikao maalumu ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriwa na wajumbe,watendaji na wataalamu wakuu wa idara zaidi ya 120.
Akitangaza maamuzi ya baraza hilo yaliyotokana  matokeo ya tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma za watumishi hao Februari 26 mwaka huu,Mstahiki Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Philip Mbogo ambaye pia ni diwani wa kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda,amewataja watumishi watakaokatwa mishahara ili kufidia hasara iliyotokana na makosa waliyoyafanya kuwa ni pamoja na Charles Ngonyani mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji, Brian Severe mkuu wa idara ya ardhi,mipango miji na maliasili, Vicent Kayombo mkuu wa idara ya elimu Shule ya Msingi, Abrahamu Kaswa afisa mipango miji, Paschal Kweya afisa afya Mazingira Manispaa ya Mpanda, Gerigori Lugarema afisa maendeleo ya jamii msaidizi.
Wengine amewataja kuwa ni Bw.Gorge Ngongolowo mhasibu mwandamizi, Albert Kiando mhandisi wa ujenzi, Victa Lutajumulwa mwalimu Mkuu elimu ya msingi daraja la pili, Focus Bilamule mhasibu Manispaa ya Mpanda, Jefu Julius  mhandisi umwagiliaji Manispaa, Said Mandua Afisa mazingira wa Manispaa ya Mpanda,Bw.Fredinandi Filimbi Mkuu wa idara sera na ufuatiliaji aliyekuwa ameshamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo alirejeshwa Manispaa Mpanda baada ya tuhuma.
Aidha Mh.Mbogo aliwataja walioshushwa vyeo kuwa ni Bw.Chamilius Luhinda Kaimu mkuu wa kitengo cha sheria Manispaa,Kibi Hamis Musaka Mhasibu Mwandamizi-Mhasibu mfumo wa EPICA ambapo pia yeye baraza limeamua atafutiwe kituo kingine cha kazi sawa na Bw.Bosko Kapinga mweka hazina wa Manispaa ambaye pia ameshushwa cheo huku baraza likiendelea kuwasiliana na mamlaka husika(TAMISEMI) ili aondolewe katika Manispaa ya Mpanda na kuhamishhiwa nje ya Manispaa.
Wakati huo huo baraza limesema kuwa haliwezi kutoa maamuzi ya kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Suleiman Lukanga anayedaiwa kutapanya zaidi ya milioni 380 katika miradi yote ya gari hewa na skimu ya umwagiliaji Kakese,kutokana na sheria kuelekeza kuwa maamuzi juu ya Mkurugenzi yanatolewa na katibu Mkuu  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ofisi ya Rais.
Mtumishi Mwingine ambaye baraza halikutoa maamuzi ni juu ya Bi.Vumilia Kakulima mkuu wa kitengo cha Manunuzi kutokana na mashauri ya tuhuma hizo kuwa tayari zipo mahakamani ambapo baraza limesema linasubiri maamuzi ya mahakama ili sheria zichukuliwe dhidi yake.
Katika hatua nyingine,Frenk Gombanila aliyekuwa ameajiriwa kama Mhudumu idara ya afya Manispaa ya Mpanda anyeadiwa kughushi vyeti na kupata ajira,amefukuzwa kazi pamoja na Shauri lake lipo kupelekwa Polisi ambapo pamoja na hali hiyo alikuwa miongoni mwa watumishi hewa Manispaa ya Mpanda.
Wakati huo huo,Yusra Marco Mtunza Kumbukumbu aliyekuwa na shtaka la utoro na hivyo kuonekana kuwa mtumishi hewa amerejeshwa kazini kutokana na kutokuwa na hatia kwa kuwa makosa yalifanyika akiwa hayupo.
Hata hivyo Mstahiki Meya Mh.Mbogo amesema kuwa ikiwa mtumishi yeyote hataridhika  na maamuzi ya baraza la madiwani anaruhusiwa kukataa rufaa.
Watumishi waliokuwa wakikaimu nafasi za waliokuwa wamesimamishwa kazi kuanzia Februari 26 mwaka huu walikuwa ni Said Mohamed Hemed mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji,Rashid Pili Idara ya elimu Msingi,Mabokera Mwakabamba kitengo cha Manunuzi,Paschal Sindani idara ya ujenzi,Juma Luhomwa mweka hazina wa Manispaa huku  Peter Charles Mkalipa atakaimu mkuu wa idara,ardhi na maliasili.
Hata hivyo katika mjadala wa nadalaza la madiwani uliodumu kwa siku mbili mfululizo usiku na mchan,takwimu kamili ya hasara iliyokana na watumishi kufanya ubadhirifu huo haijatajwa mbali na zaidi ya milioni 380 zilizokuwa zimetajwa katika mradi wa Skimu ya umwagiliaji Kakese pamoja na ununuzi hewa wa gari la kuzoa taka .
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho maalumu wamesema kuwa ikiwa pesa yote itarudishwa huenda ikapatikana pesa ya kutosha kuendesha miradi ya mendeleo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM pekee

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA