DUKA LATEKETEA KWA MOTO MPANDA,ZIMAMOTO WAENDELEA NA UCHUNGUZI WA CHANZO



DUKA moja limeteketea kwa moto na kuungua baadhi ya bidhaa zilizokuwemo ndani katika maeneo ya soko la Mpanda hoteli mkoani Katavi.

Wakizungumza baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umetokea majira ya saa tatu usiku ambapo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa katavi Bw.Nestory Konongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara  kuhudhuri semina zinazotolewa na kikosi hicho ambapo amewashauri kuwa na mitungi ya kuzimia moto katika maeneo yao ya biashara.
Katika 2016 ajali ya moto siyo ya kwanza,ambapoi mapema mwezi Februari shule moja ya sekondari nayo bweni moja la wavulana lake liliteketea katika Manispaa ya Mpanda.
Mwandishi:Rogate Tweve
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM pekee

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA