WATUMISHI HEWA MPAKA SASA MANISPAA YA MPANDA NI SIFURI PIA KUONGEZA MAGARI MAWILI KWA AJILI YA UZOAJI TAKA




Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imesema mpaka sasa haina mtumishi hewa hata mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Pombe Magufuli aziagize Halmshauri zote nchini kuhakiki watumishi hewa.



Taarifa ya uhakiki wa watumishi hewa imetolewa leo na Afisa utumishi wa halmashauri hiyo Bw.Rwezaula Justinian wakati akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la madiwani ikiwa ni siku 21 tangu ukomo wa muda wa uhakiki uliokuwa umetolewa na Rais John Magufuli.
Machi 30 mwaka huu,Mkoa wa Katavi ulibainika kuwa na watumishi hewa 21 walioisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 20 na laki saba.
Katika hatua nyingine,wiki ijayo Manispaa ya Mpanda inatarajia kupata gari la pili kwa ajili ya kuzoa taka huku gari la tatu litakalokuwa likinyonya taka maji likiwa katika hatua mbalimbali za kupatikana.
Taarifa ya kupatikana kwa magari hayo imetolewa na Kaimu mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni.
Aidha mambo mengine ambayo yamjadiliwa ni pamoja kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya  ardhi,uchongaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari,ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo yasiyokuwa na vituo hivyo,mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na uwekezaji katika sekta ya nishati ya umeme na huduma ya maji kwa wananchi ambapo kwa baadhi ya maeneo ikiwemo kata ya Mpanda Hotel suala la maji limekuwa tatizo ambapo wakazi wa kata hiyo hawana mabomba wala visima.
Kakao cha leo ni cha tatu tangu balaza la madiwani Manispaa lianze vikao vyake baada ya uchaguzi Oktoba 25.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA