MKUU WA MKOA KATAVI ATANGAZA KIYAMA KWA MAJAMBAZI



SERIKALI Mkoani Katavi imesema haitawavumilia watu au mtu atakayehusishwa na Uvunjaji wa amani ikiwemo kuteka magari Kama ilivyoripotiwa Kutokea hivi karibuni.
                                                 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga wakati wa Makabidhiano ya nyumba ya Kituo cha Polisi Kanoge na Nyumba mbili za Askari zenye uwezo wa kukaliwa na watu wane Zilijengwa kwa Msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kusaidia wakimbizi UNHCR.
Jenerali Muhuga amesema kuwa kila mtu anatakiwa kufuata sheria na kanuni za nchi na kuwataka watu kutokujihusisha na ujambazi na kusisitiza kuwa atakaye kaidi asije akalaumu kwa kile kitakachompata kutokana na kosa alilolifanya.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewaomba UNHCR kusaidia vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo vyombo vya usafiri ili kufika kwa urahisi sehemu wanazotakiwa kufika kwa wakati mwafaka.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa  UNHCR hapa nchini Bi,Chavisa Kapaya Kutoka Nchini Zambia ameishukuru Tanzania kwa Kuonyesha Ujirani mwema wa Kuwapa hifadhi wakimbizi Kutoka nchini Burundi Pamoja  na Kuwapa Uraia wa Tanzania.
Aidha amewakumbusha raia wapya kuendelea kutii sheria za nchi ili kuimarisha usalama wan chi.
Kwa upande wa wakazi wa Kanoge yaliyokuwa Makambi ya wakimbizi Kabla ya kupewa uraia,wameishukuru UNHCR Kutimizi ahadi ya Ujenzi wa Kituo cha polisi ambacho wamesema Kuwepo kwa kituo hicho itaimarisha hali ya Usalama katika Makazi yao.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri :Issack Gerald

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA